Kusanyikeni Viumbe
| Kusanyikeni Viumbe | |
|---|---|
| Performed by | St. Cecilia Zimmerman |
| Category | Entrance / Mwanzo |
| Composer | J. C. Shomaly |
| Views | 3,981 |
Kusanyikeni Viumbe Lyrics
Kusanyikeni kusanyikeni viumbe wake Bwana
Tumsifuni Mungu wetu mwema aliyeumba vyote *2
Amsheni vinanda leteni na zeze na nyimbo nzuri
Zenye kupendeza msifuni Mungu*2- Kaumba nchi, kaumba wanyama,
Binadamu na fikira zake
Lipi lisilomtegemea yeye iwe mvua ama ni jua - Kawapa wengine mali nyingi sana,
Wengine ni dhiki tupu
Ili wote wategemeane kwa kile alichowajalia