Uzuri wa Yesu
Uzuri wa Yesu | |
---|---|
Choir | St. Joseph Migori |
Album | Uzuri wa Yesu |
Category | Injili na Miito (Gospel) |
Composer | Alfred Ossonga |
Uzuri wa Yesu Lyrics
{ Kwa imani yangu, matendo na maneno
Nihubiri neno la Mungu siku zote
Nipeleke neno la Mungu pande zote
Mataifa wanangojea neno hilo } *2
1. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Kwa ajili ya uzuri wake wa daima
Uzuri wake Yesu usio na kiasi
Nitende yote mema nifanane na Yesu.
2. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Nimeyasahau maneno ya zamani
Ya kale yamepita shetani ameshindwa
Nimempata Yesu natembea na yeye
3. Kwa ajili yake Yesu Kristu Bwana wangu
Kwa ajili ya uzuri wake wa daima
Nakaza mwendo sana nipeleke ujumbe
Ujumbe wake Yesu kwa mataifa yote
4. Kwa imani pia matendo na maneno
Kwa upendo pia upole na kiasi,
Nimeweka msingi imara kwake Yesu
Usiotikisika daima siku zote
Favorite Catholic Skiza Tunes
SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.
Title | SKIZA ID |
Cha Kutumaini Sina | 5814855 |
Roho Yangu na Ikuimbie | 5814859 |
Nikupe Nini Mungu Wangu | 7482438 |
Sasa Wakati Umefika | 7482439 |
Nitakwenda Mimi Mwenyewe | 7482440 |
Zaeni Matunda Mema | 5814860 |
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu | 7482444 |
Huniongoza Mwokozi | 5814856 |
Utukuzwe Ewe Baba | 7482441 |
Tazama Tazama | 7482442 |