Login | Register

Sauti za Kuimba

Kwa Nyimbo Nzuri Lyrics

KWA NYIMBO NZURI

@ Alfred Ossonga

 1. Kwa nyimbo nzuri za furaha,
  njooni nyote mbele za Bwana
  Kwa shangwe na vigelegele,
  tumwimbie Mfalme wetu

  Mataifa yote simameni mbele zake Bwana,
  Makabila yote njoni leo nazo ngoma zenu
  Chezeni mbele za Bwana!
  { Wajaluo na waimbe nyimbo
  Wamasai na waruke juu
  Wabaluhyia na wapige ngoma
  Wakikuyu na wacheze sana,
  Watu wote sisimukeni,
  Shangwe nderemo na kelele, pigeni makofi } *2

 2. Vinanda vifijo kelele,
  makofi machezo nderemo
  Kusifu kweli kwawapasa,
  enyi wanyofu wa moyo
 3. Pigieni Mungu kelele,
  imbeni utukufu wake
  Tukuzeni sifa za Mungu,
  tangazeni matendo yake
 4. Shukuruni Bwana kwa zeze,
  kwa kinanda cha nyuzi kumi
  Mfanyieni Bwana shangwe,
  mtumikieni kwa furaha
Kwa Nyimbo Nzuri
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYEntrance / Mwanzo
 • Comments