Leo Tumepata Mfalme Lyrics

LEO TUMEPATA MFALME

{ [ v ] Leo tumepata mfalme
[ w ] Leo tumepata mfalme, ndiye mtoto Yesu } *2
{ Utukufu juu mbinguni, na amani duniani (kote)
Kwa watu wenye mapenzi wenye mapenzi mema } *2

 1. Malaika kawambia, wachungaji kondeni
  Amkeni upesi, twende Bethlehem
 2. Leo mji wa Daudi, kazaliwa mfalme
  Jina lake Emanueli, Mungu pamoja nasi
 3. Malaika kawaambia, wale mamajusi
  Kutoka mashariki, kazaliwa mfalme.
 4. Mtaona hiyo nyota, kutoka mashariki
  Ndiyo itawaongoza, alipo mfalme.
Leo Tumepata Mfalme
CHOIROur Lady of Fatima Kongowea
ALBUMKila Mwenye Pumzi (vol 4)
CATEGORYNoeli (Christmas Carols)
 • Comments