Lo Bwana! Mbona Unameza Mate?
Lo Bwana! Mbona Unameza Mate? |
---|
Performed by | - |
Category | Harusi |
Views | 3,618 |
Lo Bwana! Mbona Unameza Mate? Lyrics
- Lo Bwana mbona unameza mate na hakuna chakula
Kwani wewe huna macho huoni ile keki
Iiliyo pale mbele kumbe tutashiba
Enyi maarusi kateni keki tuanzeni kula
Kwani watu wameanza kunyongwana mate
Lakini kateni keki kwa utaratibu
Isije ikaanguka nasi tukakosa kula
Kwani watu wasipoonja keki hiyo
Hawatatambua kwamba hii ilikuwa ni arusi
- Mwenzangu haraka sasa ya nini mbona wanikanyaga
Kama keki hutapata mahali we ulipo
Kwa hivyo jitulize, wacha kunifinya
- Kumbuka enyi maharusi keki hii ina maana kubwa
Kwani keki ni ishara ya kuwaunganisha
Muwe kitu kimoja msaidiane