Lo Kaburi Wazi
Lo Kaburi Wazi | |
---|---|
Performed by | Our Lady(Star of the Sea) Kenya Navy |
Album | Tumeandamana |
Category | Pasaka (Easter) |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 9,830 |
Lo Kaburi Wazi Lyrics
- Mama Maria tuambie, uliona nini njiani
Nanyi mitume tueleze mliyemkuta pangoni
{ (kweli) Ni malaika, toka mbinguni
Tulimwona pale kaburini } *2Lo! Kaburi wazi!
Hayumo, ni mzima, hayumo, amefufuka *2
Lo! Kashinda kifo!
Mauti, yameshindwa, tuimbe, tushangilie *2 - Amefufuka ni hakika, amefufuka kweli kweli
Dunia nzima ifurahi, hata mbinguni wanaimba
{ (kweli) Twimbe tucheze, twimbe turuke,
Twimbe sana , twimbe aleluya } *2 - Nguvu za shetani kashinda, kamba za mauti amekata
Ngome ya kuzimu kavunja, kaburi za wafu zafunguka
{ (kweli) Simba wa Yuda, amenguruma,
Walinzi nao mbio watimua } *2 - Ameondoka kaburini, aelekea Galilaya
Nasi twendeni hima hima, twendeni kule Galilaya
{ (kweli) Twendeni leo, twendeni sote,
Tumwimbie nyimbo za ushindi } *2 - Tumekombolewa kwa damu, damu yake Mwanakondoo
Lango la mbingu liko wazi, kwao waliokombolewa
{ (kweli) Tukimwamini, tutaingia,
Tutaishi na Mungu milele } *2