Maajabu Ya Mungu
   
    
     
         
          
            Maajabu Ya Mungu Lyrics
 
             
            
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa rangi mbalimbali *4
 Wengine ni weusi, wengine ni weupe,
 Wengine ni wekunde, wengine ni wekundu,
 Wote ni wa Mungu, wote
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kimo mbalimbali *4
 Wengine ni warefu wengine ni wafupi,
 Wengine ni wanene, wengine ni wembamba
 Wote ni wa Mungu, wote
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa wito mbalimbali *4
 Wengine ni wa ndoa, wengine ni watawa,
 Wengine makuhani, wengine ni wa ndoa
 Wote ni wa Mungu, wote
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kazi mbalimbali *4
 Wengine makarani, wengine ni polisi
 Wengine waalimu, wengine makarani
 Wote ni wa Mungu, wote
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa umri mbalimbali *4
 Wengine ni watoto, wengine ni vijana,
 Wengine ni wa kati, wengine ni wazee
 Wote ni wa Mungu, wote
- Maajabu ya Mungu kaumba watu wa sifa mbalimbali *4
 Wengine ni hekima, wengine ni busara,
 Wengine polepole, wengine ni haraka
 Wote ni wa Mungu, wote