Maajabu Ya Mungu

Maajabu Ya Mungu
ChoirSt. Cecilia Mirerani
AlbumMaajabu ya Mungu
CategoryTafakari
ComposerFr. Aloyce Msigwa

Maajabu Ya Mungu Lyrics

 1. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa rangi mbalimbali *4
  Wengine ni weusi, wengine ni weupe,
  Wengine ni wekunde, wengine ni wekundu,
  Wote ni wa Mungu, wote
 2. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kimo mbalimbali *4
  Wengine ni warefu wengine ni wafupi,
  Wengine ni wanene, wengine ni wembamba
  Wote ni wa Mungu, wote
 3. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa wito mbalimbali *4
  Wengine ni wa ndoa, wengine ni watawa,
  Wengine makuhani, wengine ni wa ndoa
  Wote ni wa Mungu, wote
 4. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa kazi mbalimbali *4
  Wengine makarani, wengine ni polisi
  Wengine waalimu, wengine makarani
  Wote ni wa Mungu, wote
 5. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa umri mbalimbali *4
  Wengine ni watoto, wengine ni vijana,
  Wengine ni wa kati, wengine ni wazee
  Wote ni wa Mungu, wote
 6. Maajabu ya Mungu kaumba watu wa sifa mbalimbali *4
  Wengine ni hekima, wengine ni busara,
  Wengine polepole, wengine ni haraka
  Wote ni wa Mungu, wote