Maisha Yangu
Maisha Yangu | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | G. Tesha |
Views | 20,662 |
Maisha Yangu Lyrics
Maisha yangu
Maisha yangu ni Yesu Kristu (Bwana wangu)
Uhai wangu
Uhai wangu ni Yesu Kristu (Mwokozi) } * 2
{ (Haya)
/s/ Enyi wapenzi wa Bwana njoni mjiunge nami, tumsifu Bwana Mungu wetu
/a/ Enyi wapenzi wa Bwana wangu njoni pamoja nami, tumsifu Bwana Mungu wetu
/t/ Enyi wapenzi wa Bwana wangu njoni mjiunge nami tumsifu Bwana Mungu wetu
/b/ Enyi wapenzi wa Bwana tumwimbie Bwana pamoja nami,
Tumsifu Bwana Mungu wetu } *2- Anajua kula yangu, anajua vaa yangu
Anajua niendapo, anajua nitendalo
Maisha yangu yamo mikononi mwake - Anajua mwanzo wangu anajua mwisho wangu
Anajua nilalapo, anajua niamkapo
Tegemeo la maisha yangu ni Yesu - Ananipa kila kitu, ananipa na uhai
Yeye anikumbatia kama mwana wake mpenzi
Pumzi zangu zatoka kwake Bwana wangu - Upendo wake ajabu, huruma yake amini
Msamaha wake kwangu, daima ni wa milele
Ama kweli maisha yangu ni kwa Yesu