Mama Akaitika

Mama Akaitika
ChoirKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumNakaza Mwendo (Vol 19-20)
CategoryBikira Maria
ComposerBernard Mukasa

Mama Akaitika Lyrics

 1. Hatari ikaja nikageuka mbio kumlilia -
  Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
  Akaifungua mikono yake myema kanidaka -
  Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee
  Nikalaza kichwa kifuani kwa mama nikihema-
  Nikaita mama naye akaitika mwanangu ee

  |t| Mama anayenipenda, Maria ananijali,
  Popote ninapokwenda, mimi niko salama,
  Nitakimbilia hapo hapo kwa mama wa
  Nitakimbilia hapo hapo kwa mama wa upendo

  |w| Mama yangu Maria nyumba ya salama
  Mama yangu Maria nyumba ya salama
  A hapo hapo kwa mama wa upendo
  Ni hapo hapo kwa mama wa upendo

 2. Wenye nguvu zao walibeba silaha, kupigana -
  Wakapigania ndani ya nyumba yetu, hatari kuu
  Wakazidiana paa wakalipua,tumekwisha -
 3. Kwenye familia migogoro ya ndoa shida tupu -
  Watoto wakawa na maadili duni, balaa tu -
  Na magonjwa lundo uchumi hohehahe, taabu tu
 4. Bibi yangu Eva alizaa laana duniani -
  Mama yangu mwema akazaa wokovu,wa milele
  Nkakabidhiwa niwe mwanaye naye, mamangu ee -
 5. Uovu wa watu ulishika hatamu kila kona -
  Amani ikawa ndoto ya jua kali haipo ee -
  Hofu na mashaka vikafunika nchi,hatari kuu -
 6. Baba wa kanisa akaniita shime tujiunge-
  Tusali rozari tumlilie mama wa amani -
  Atatusikia ataushusha mkono wa Yesu -