Twakuomba Mama Maria
Twakuomba Mama Maria Lyrics
- Mama Maria Mwombezi wetu,
mama wa neema na hu-ruma
Tusikilize Mama wa Yesu,
tusikilize wakosefu
Twakuomba Mama Maria,
kwa Mwanao Mama tuombee
Sala zetu Mama Maria,
kwa Mwanao mama zifikishe
Nyoyo zetu Mama Maria,
zatamani kufika mbinguni
- Mama Maria uliye mwema,
tuliza nyoyo zetu wanao
Tunaposhindwa tusaidie,
tusije baki katika giza
- Mama Maria twakuamini,
mama wa Mungu msaada wetu
Matumaini yetu ni kwako,
katika shida tusimamie
- Mama Maria usituache,
umpelekee Bwana maombi
Atubariki wenye mashaka,
tupate uzima wa milele