Mama Mzazi wa Mungu Lyrics

MAMA MZAZI WA MUNGU

 1. Mama mzazi wa Mungu mama twakushangilia
  Wewe ndiwe mama yetu, Mama mwengine hatuna

  Ewe Maria mama, tuombee kwa mwanao
  Ewe Maria mama, tuombee kwa mwanao

 2. Maria twakupongeza, kwa kuwa u mama yetu
  Tulegeze ukaidi, na tuwe wanyenyekevu
 3. Pale msalabani juu, mwanao kakupeana
  Akawambia Yohane, tazama huyu mama yako
 4. Maria anatuonya, kama Mama wa Kanisa
  Anasema dunia hii, dunia imechafuka
Mama Mzazi wa Mungu
CHOIR
CATEGORYBikira Maria
 • Comments