Mama Pale Msalabani
| Mama Pale Msalabani | |
|---|---|
| Performed by | - | 
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) | 
| Views | 15,934 | 
Mama Pale Msalabani Lyrics
- Mama pale msalabani, macho yatoka machozi
 Akimwona mwanaye, kweli ni huzuni kubwa
- Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,
 Ukampenya moyowe
- Mwenye moyo mgumu nani, asimhurumie basi
 Mama amlilia mwana
- Ewe Mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
 Moyo wangu mwenye dhambi
- Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
 Pamoja na ukombozi
- Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
 Wa uchungu na msiba
- Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
 Ewe bikira mwema
- Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
 Ewe Mwokozi wangu
- Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
 Niende kwako Mungu
Mama Pale Msalabani (alternative)
- Mama pale msalabani, macho yatoka machozi
 Akimwona mwanaye, akimwona mwanaye
- Kweli vile akilia, uchungu kama upanga,
 Ukampenya moyowe, ukampenya moyowe
- Mwenye moyo mgumu, nani asimhurumie basi
 Mama mlilia mwana, mama mlilia mwana?
- Ewe mama mtakatifu, usulubiwe na Yesu
 Moyo wangu mwenye dhambi, moyo wangu mwenye dhambi
- Naye Mwokozi niteswe, na madonda nigawie
 Pamoja na ukombozi, pamoja na ukombozi
- Nisimame msalabani, niwe nami wako mwenzi
 Wa uchungu na msiba, wa uchungu na msiba
- Nisianguke motoni, uniwie msimamizi,
 Ewe Bikira mwema, ewe bikira mwema
- Msikilize mama yako, niponye siku ya mwisho
 Ewe Mwokozi wangu, ewe Mwokozi wangu
- Nitakapokufa mimi, upokee roho basi
 Niende kwako Mungu, niende kwako Mungu
 
  
         
                            