Mataifa ya Ulimwengu
Mataifa ya Ulimwengu | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Ikatetemeka Nchi (Vol 3) |
Category | Thanksgiving / Shukrani |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 13,448 |
Mataifa ya Ulimwengu Lyrics
{ Mataifa yote ya ulimwengu
Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) } *2
{ Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru
Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi
Ninashukuru Mungu wangu leo
Na nyimbo nzuri ninaimba ili kesho nayo niwe salama
Nazo sifa zako, nitangaze pote } *2- Uamkapo asubuhi ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda usiku wenye giza tororo
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha - Ufikapo safari yako ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda na ajali za barabarani
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha - Shikaneni mikono sasa yote muinyanyue juu
Semeni kwa shangwe na mbwebwe maneno haya kwa furaha
Ameweza Bwana Mungu kweli ameweza ameweza - Akina mama simameni sasa mpige vigelegele
Na kina Baba nyanyukeni mpige makofi ya shangwe
Muimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha