Mataifa ya Ulimwengu

Mataifa ya Ulimwengu
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryThanksgiving / Shukrani
ComposerJ. C. Shomaly
Musical Notes
Timesignature3 8
MusickeyG Major

Mataifa ya Ulimwengu Lyrics


{ Mataifa yote ya ulimwengu
Yatakusujudia ee Mungu (Mungu Baba) } *2
{ Mema uliyonitendea Mungu wangu ninashukuru
Jana leo nimeamka kesho sijui itakuwa vipi
Ninashukuru Mungu wangu leo
Na nyimbo nzuri ninaimba ili kesho nayo niwe salama
Nazo sifa zako, nitangaze pote } *2


1. Uamkapo asubuhi ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda usiku wenye giza tororo
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha

2. Ufikapo safari yako ndugu yangu, umshukuru Mungu
Kwa jinsi alivyokulinda na ajali za barabarani
Uimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha

3. Shikaneni mikono sasa yote muinyanyue juu
Semeni kwa shangwe na mbwebwe maneno haya kwa furaha
Ameweza Bwana Mungu kweli ameweza ameweza

4. Akina mama simameni sasa mpige vigelegele
Na kina Baba nyanyukeni mpige makofi ya shangwe
Muimbe kwa furaha na kuchezacheza kwa madaha

Favorite Catholic Skiza Tunes

SMS the Skiza ID to 811 to get the song as your Skiza tune.

TitleSKIZA ID
Cha Kutumaini Sina 5814855
Roho Yangu na Ikuimbie 5814859
Nikupe Nini Mungu Wangu 7482438
Sasa Wakati Umefika 7482439
Nitakwenda Mimi Mwenyewe 7482440
Zaeni Matunda Mema 5814860
Bwana Kama Wewe Ungehesabu Maovu Yetu 7482444
Huniongoza Mwokozi 5814856
Utukuzwe Ewe Baba 7482441
Tazama Tazama 7482442