Mbegu Nyingine

Mbegu Nyingine
Performed bySt. Benedict Rapogi
AlbumMbegu Nyingine (Vol 2)
CategoryZaburi
ComposerOchieng Odongo
Views15,527

Mbegu Nyingine Lyrics

  1. { [s] Mbegu nyingine zikaanguka
    [w] Mbegu nyingine (zikaanguka)
    Mbegu nyingine zikaanguka penye udongo mzuri! } *2
    Zikamea, zikamea na tena zikazaa *2
  2. Umeijalia nchi na kuistawisha,
    Mto wako Bwana umejaa maji mazuri
  3. Wewe unawaruzuku watu wote nafaka,
    Na umeuvika mwaka taji ya wema wako
  4. Pia na matuta yake maji umeyajaza,
    Wapasawazisha popote palipoinuka
  5. Wailainisha nchi kwa manyunyu ee Bwana,
    Hata na mimea yake wewe waibariki
  6. Kila upitapo kweli pamejaa unono,
    Huyadondokeza na malisho yote nyikani
  7. Na vilima vyote vajifunga nayo furaha,
    Na malisho yote yamevikwa nao kondoo