Mbinguni Kutakuwa Raha
Mbinguni Kutakuwa Raha | |
---|---|
Alt Title | Ole Wenu |
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Mbinguni Kutakuwa Raha (Vol 4) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 10,973 |
Mbinguni Kutakuwa Raha Lyrics
Nakiri kuwasimulieni na kuwapa siri hii hakika
Mbinguni kutakuwa raha kwa wale wote watakaofika
Hili jambo labidi nitamke kwani nimefikiria hakika
Hakutakuwa rushwa hongo, hirizi wala mlango wa kona,
Heri waliochaguliwa kufurahi na Mwanakondoo
Waliovumilia shida, starehe na anasa za nchi
Ole wenu (ole), ole wenu (ole) ole wenu mnaocheka sasa
Mtalia (nyinyi) mtalia (nyinyi) mtalia na kuomboleza
Ole wenu (ole) Ole wenu (ole) ole wenu mpiganao sasa
Fainali yake inakuja mshahara ni mauti- Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao rushwa
Siku zinakuja nayo rushwa pia itakuhukumu - Ole wenu ole wenu nyinyi mpendao wizi
Siku zinakuja vyote ulivyoiba utarudisha - Furahini furahini nyinyi mpendao haki
Siku zinakuja mtakuwa wakuu wa wafalme - Furahini furahini mtesekao kwa dhiki
Siku zinakuja ufalme wote utakuwa ni wenu