Mbona Nahangaika
| Mbona Nahangaika | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
| Album | Ikatetemeka Nchi (Vol 3) |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | D. Mdodo |
| Views | 8,090 |
Mbona Nahangaika Lyrics
{ Mbona nahangaika, mkiwa mimi,
Sina hata wa kunifuta machozi } *2
Ni aibu gani iliyonitanda,
Najuta hata siku ya kuzaliwa kwangu
{ Maskini mimi, nitakuwa mgeni wa nani,
Nakulilia e Mungu uniokoe } *2- Taabu na matatizo yanisonga mimi
Shida nazo karaha zanisumbua mimi,
Mungu ufanye hima uniokoe. - Nimeugua nikilalama, mnyonge mimi,
Sina rafiki wala mtetezi, mkiwa mimi
Wote wamenigeuka kuniwinda, - Kila waliwazalo juu yangu ni baya,
Kuugua kwangu kumbe ni furaha kwao
Walitaka nife nisahaulike.