Mbona Nahangaika

Mbona Nahangaika
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumIkatetemeka Nchi (Vol 3)
CategoryKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
ComposerD. Mdodo
Views7,120

Mbona Nahangaika Lyrics

  1. { Mbona nahangaika, mkiwa mimi,
    Sina hata wa kunifuta machozi } *2
    Ni aibu gani iliyonitanda,
    Najuta hata siku ya kuzaliwa kwangu
    { Maskini mimi, nitakuwa mgeni wa nani,
    Nakulilia e Mungu uniokoe } *2

  2. Taabu na matatizo yanisonga mimi
    Shida nazo karaha zanisumbua mimi,
    Mungu ufanye hima uniokoe.
  3. Nimeugua nikilalama, mnyonge mimi,
    Sina rafiki wala mtetezi, mkiwa mimi
    Wote wamenigeuka kuniwinda,
  4. Kila waliwazalo juu yangu ni baya,
    Kuugua kwangu kumbe ni furaha kwao
    Walitaka nife nisahaulike.