Mfalme wa Amani
Mfalme wa Amani | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Cathedral Dar-es-Salaam |
Category | Jumapili ya Matawi (Palm Sunday) |
Composer | (traditional) |
Views | 16,663 |
Mfalme wa Amani Lyrics
- Mfalme wa amani mpeni heshima,
Yerusalem mjini anaingia
Na unyenyekeo na upole mkuu
Anapanda punda Mwana wa Mungu.Hosana juu, hosana Juu, hosana juu.
- Njooni Mahebruni, njooni watoto,
Leteni matawi ya kumsalimu.
Mwana wa Daudi kweli Masiya
Anakuja kwenu mwenye huruma. - Tandikeni nguo miguuni pake,
Imbeni zaburi, shangilieni.
Mbarikiwa huyu ajaye kwetu
Kwa Jina la Bwana Mkombozi mkuu. - Ufurahi sana, we` Yerusalem
Yule wamwabudu roho za mbingu.
Na huruma pale anakujia,
Haki na amani akuletea. - Ndimi za wachanga zafumbulia,
Kwa mwujiza sifa yake Masiya
Na makundi yote ya malaika
Sifa na heshima wanamtolea.