Mimi Mzabibu wa Kweli
Mimi Mzabibu wa Kweli | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | Haya Tazameni (Vol 21) |
Category | Mafundisho ya Yesu |
Composer | Hanga |
Views | 12,401 |
Mimi Mzabibu wa Kweli Lyrics
[s] Mimi mzabibu wa kweli, mimi mzabibu wa kweli,
Nanyi m matawi yangu, Baba yangu ni mkulima,
Mwenye kutunza shamba lake } *2
[s] Tawi lile lisilozaa
Baba yangu huliondoa, na kuliteketeza moto,
[s] Tawi lile linalozaa
Baba yangu hulisafisha, lidumu katika kuzaa
Hayo - hayo ni maneno ya Bwana Yesu }*2- Nyinyi mmekwisha, kuwa wasafi,
Kwa sababu ya neno, nililowaambia
Kaeni nami, ndani yangu,
Na mimi na mimi na mimi ndani yenu - Akaaye ndani yangu, huyo atazaa
Kwani nje yangu, hataweza kuzaa
Kama vile nje ya mzabibu,
Tawi halitaweza kamwe kuzaa. - Maneno yangu yakikaa ndani mwenu,
Ombeni lolote mtatendewa
Naye Baba yangu atatukuzwa,
Na nyinyi mtakuwa wanafunzi wangu