Mimi Ndimi Chakula
Mimi Ndimi Chakula Lyrics
Mimi ndimi chakula kilichoshuka
kutoka mbinguni, asema Bwana
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu
Ataishi, ataishi milele na milele asema Bwana
- Njooni kwangu mnaolemewa na mizigo
Njooni kwangu nitawapumzisha
- Njooni kwangu mimi ni chakula cha kweli
Njooni kwangu njooni niwashibishe
- Njooni kwangu mimi ni kinywaji cha kweli
Njooni kwangu nitawaburudisha
- Njooni kwangu mimi ndimi uzima wa kweli
Njooni kwangu mtapata wokovu
- Njooni kwangu mimi ndimi wokovu wa kweli
Njooni kwangu mtapata wokovu
- Njooni kwangu mimi ndimi uhai wa kweli
Njooni kwangu mtaishi milele