Mimi Ndimi Chakula

Mimi Ndimi Chakula
ChoirTBA
CategoryEkaristia (Eucharist)

Mimi Ndimi Chakula Lyrics

Mimi ndimi chakula kilichoshuka
kutoka mbinguni, asema Bwana
Aulaye mwili wangu na kuinywa damu yangu
Ataishi, ataishi milele na milele asema Bwana

 1. Njooni kwangu mnaolemewa na mizigo
  Njooni kwangu nitawapumzisha
 2. Njooni kwangu mimi ni chakula cha kweli
  Njooni kwangu njooni niwashibishe
 3. Njooni kwangu mimi ni kinywaji cha kweli
  Njooni kwangu nitawaburudisha
 4. Njooni kwangu mimi ndimi uzima wa kweli
  Njooni kwangu mtapata wokovu
 5. Njooni kwangu mimi ndimi wokovu wa kweli
  Njooni kwangu mtapata wokovu
 6. Njooni kwangu mimi ndimi uhai wa kweli
  Njooni kwangu mtaishi milele