Mimi Ndimi Mzabibu
Mimi Ndimi Mzabibu | |
---|---|
Performed by | St. Joseph Migori |
Album | Hodi Hodi |
Category | Mafundisho ya Yesu |
Composer | Alfred Ossonga |
Views | 24,787 |
Mimi Ndimi Mzabibu Lyrics
{ Mimi ndimi mzabibu wa kweli,
Mimi ni mzabibu wa kweli
Nanyi m matawi yangu, asema Bwana } *2- [ b ] Na Baba yangu ndiye mkulima,
Kila tawi lisilozaa, Baba hulikata
Nalo tawi lizaalo, Baba hulisafisha, ili lizidi kuzaa - Kaeni nyote ndani yangu mimi,
Nami nikae ndani yenu, kwa maana mtu
Akaaye ndani yangu, nami ndani yake, huyo huzaa matunda - Mimi ni mti mti wa zabibu,
Nanyi ndinyi matawi ya mzabibu huu
Tawi linalojitenga, kutoka kwa mti huu, hunyauka tena hufa