Mimi Nikushukuruje
| Mimi Nikushukuruje | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) | 
| Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) | 
| Category | Thanksgiving / Shukrani | 
| Composer | J. C. Shomaly | 
| Views | 8,455 | 
Mimi Nikushukuruje Lyrics
- [ s ] Mimi nikushukuruje Bwana -
 [ w ] Mungu wangu nikushukuruje
 [ s ] Kwa mema mengi umenijalia -
 [ w ] Mungu wangu nikushukuruje
 { Umenipa uhai napendeza, umenipa nyumba pia watoto,
 Nafikiri nikushukuruje Mungu wangu ninasema asante }*2
- Umenijalia mali, nikutumikie wewe
 Niwagawie maskini, wajane pia yatima
- Umenipa na akili nitambue mambo yote
 Mabaya niweke kando, mazuri nitumikie.
- Umenipa na chakula kilichotoka mbinguni
 Chenye kushibisha roho, ili nifike mbinguni.
 
  
         
                            