Mimi Nimewachagua Ninyi
| Mimi Nimewachagua Ninyi |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Tafakari |
| Composer | Fr. L. Malema |
| Views | 8,314 |
Mimi Nimewachagua Ninyi Lyrics
{ Mimi nimewachagua ninyi duniani
Mimi nimewachagua duniani } *2
{ Ili mpate kwenda kuzaa matunda
Na matunda yenu yadumu, yadumu, siku zote } *2
- (Yesu alisema) si ninyi mlionichagua mimi,
Bali ni mimi nimewachagua ninyi
- Nami nimewaweka kwenda kuzaa matunda
Na matunda yenu yadumu
Ili kwamba lolote mumwombalo Baba
Kwa jina langu awapeni
- Iwapo ulimwengu utawachukia
Mjue kwamba umenichukia mimi
kabla ya kuwachukia ninyi.
- Kama mngekuwa wa ulimwengu,
Ulimwengu ungeliwapenda
Lakini kwa kuwa ninyi si wa ulimwengu,
Bali mimi nimewachagua katika ulimwengu,
Kwa sababu hiyo ulimwengu utawachukia.