Mke Mwema
| Mke Mwema |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Harusi |
| Views | 8,587 |
Mke Mwema Lyrics
Mke mwema, mke ni nani, awezaye kumuona
Kima chake, kima chapita, kima cha marijani
{Moyo wa mumewe unamwamini,
Wala hatakosa kupata mapato *2}
- Humtendea mema wala si mabaya,
Siku zote zote za maisha yake
- Hutafuta sufu sufu na kitani,
Taa yake haizimiki usiku
- Huwakunjulia maskini mikono,
Huwanyooshea wahitaji mikono
- Mwanamke yule amchaye Bwana,
Na huyo ndiye atakayesifiwa
- Mpe mapato ya mikono yake,
Basi na kazi yake yamsifu
~ (Prov 31)