Moyo Wangu Unakutamani

Moyo Wangu Unakutamani
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumTazameni Miujiza (Vol 2)
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerBernard Kiundi
Views8,502

Moyo Wangu Unakutamani Lyrics

  1. { Moyo wangu unakutamani,
    Moyo wangu unakutamani Mungu wangu } *2
    { Kwa sauti nzuri mimi nikuimbie ee Mungu wangu,
    Nitangaze sifa zako milele na hata milele } *2

  2. Nikuambie nini Bwana, ujue ninakupenda
    Moyo wangu umekuambia uso wako nitautafuta
    Usinifiche uso wako ee Mungu Muumba wangu
  3. Umenitendea mambo mengi, makubwa ya kushangaza
    Sasa mimi nitazitangaza fadhili zako Bwana wangu
    Asubuhi hata usiku ee Mungu nitakusifu
  4. Nibariki ee Mungu wangu, siku zote za maisha yangu
    Nikusifu wewe daima nitangaze uwezo wako
    Usiwe mbali Mungu wangu naomba usiniache.