Moyo Wangu Unakutamani

Moyo Wangu Unakutamani
ChoirSt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumTazameni Miujiza (Vol 2)
CategoryEkaristia (Eucharist)
ComposerBernard Kiundi
Musical Notes
Time Signature2
4
Music KeyG Major

Moyo Wangu Unakutamani Lyrics

{ Moyo wangu unakutamani,
Moyo wangu unakutamani Mungu wangu } *2
{ Kwa sauti nzuri mimi nikuimbie ee Mungu wangu,
Nitangaze sifa zako milele na hata milele } *2

 1. Nikuambie nini Bwana, ujue ninakupenda
  Moyo wangu umekuambia uso wako nitautafuta
  Usinifiche uso wako ee Mungu Muumba wangu
 2. Umenitendea mambo mengi, makubwa ya kushangaza
  Sasa mimi nitazitangaza fadhili zako Bwana wangu
  Asubuhi hata usiku ee Mungu nitakusifu
 3. Nibariki ee Mungu wangu, siku zote za maisha yangu
  Nikusifu wewe daima nitangaze uwezo wako
  Usiwe mbali Mungu wangu naomba usiniache.