Moyo Wangu Wamtukuza
Moyo Wangu Wamtukuza | |
---|---|
Performed by | - |
Category | Bikira Maria |
Views | 47,127 |
Moyo Wangu Wamtukuza Lyrics
{(Moyo) Moyo wangu wamtukuza Bwana
(Roho) Roho yangu inafurahi }*2- Kwa kuwa amemwangalia, kwa huruma mtumishi wake
Hivyo tangu sasa watu wote, wataniita mwenye heri - Kwa sababu Mwenyezi Mungu, amenifanyia makuu
Jina lake ni takatifu, - Huruma yake ni kwa wote, wote wale wanaomcha
Kizazi hata na kizazi, - Huyatenda mambo makuu, kwa nguvu za mkono wake
Wenye kiburi hutawanywa, - Hushusha wote wenye vyeo, kutoka vitini vya enzi
Nao wale wanyenyekevu, wote hao huwainua - Huwashibisha wenye njaa, na matajiri huwaacha
Waende mikono mitupu, - Hulilinda taifa lake, teule la mtumishi wake
Akikumbuka huruma yake, - Kama alivyowaahidia, babu zetu kuwaahidia
Ibrahimu na mzao wake, - Atukuzwe Baba na Mwana, naye Roho Mtakatifu
Leo kesho hata milele, kwa shangwe milele amina
~Lk. 1:39-55
Also recorded by Thika Catholic