Mpendane Daima

Mpendane Daima
Performed bySt. Joseph Migori
AlbumNitachezacheza
CategoryHarusi
ComposerAlfred Ossonga
Views5,435

Mpendane Daima Lyrics

 1. Mungu akaona si vyema mtu huyu awe peke yake
  Nitamfanyia mwenzake yule wanafanana naye
  Akaumba mwanamke, kamleta kwake mwanamume waishi pamoja

  { Ewe Bwana - mpokee mke wako tangu leo
  Ewe Bibi - mpokee mume wako tangu leo
  Muishi nyote pamoja, mpendane daima
  Msitengane daima, msivunje agano } *2

 2. Mungu akawapa uwezo watawale viumbe vyote
  Mungu akasema zaeni muijaze dunia kwa watu
  Baraka za Mungu Baba, zimewashukia tangu leo zaeni matunda
 3. Ewe mwanamume mpende mke wako kwa moyo wote
  Nawe mwanamke heshimu mume wako mtii daima,
  Ndoa ni maagano, kati ya watu wawili wapendanao
 4. Nyumba yenu iwe hekalu lake Mungu kanisa ndogo
  Nyumba ya amani upole na furaha nyumba ya sala
  Mungu ameunganisha mwanadamu asitenganishe daima dawamu