Mpende Adui
Mpende Adui |
---|
Alt Title | Amri ya Mapendo |
Performed by | St. Cecilia Kajiado |
Album | Imani Kipimo |
Category | Love |
Composer | M. Z. Yohana |
Views | 7,533 |
Mpende Adui Lyrics
- Bwana Yesu alituachia amri ya mapendo
Ili tupendane kama yeye alivyotupenda
Tena akasema, akasisitiza,
Mpende jirani, kama nafsi yako
{ Mpende - adui yako
Mpende - muombee neema
Mpende - adui yako
Mpende - muombee Baraka } *2
- Sisi tulivyoumbwa wanadamu hatulingani
Kwa tabia kwa maisha hata kwa matendo yetu
Wapo wa hekima, wasemao ukweli,
Na wenye kiburi, wasio na busara
- Hata ukinyanyaswa jitahidi kuvumilia
Usiwe mwenye ghadhabu ukalipiza kisasi
Ukihuzunishwa, mkimbilie Yesu,
Atakupa faraja, heri na fanaka
- Usikumbuke ubaya uliokwisha tendewa,
Hiyo itakuwa njia ya kukaribisha chuki
Ukisha samehe, usahau yote,
Ukatae yote, yasiyo ya hekima