Mpigieni Bwana
| Mpigieni Bwana |
|---|
| Performed by | - |
| Category | Zaburi |
| Views | 8,174 |
Mpigieni Bwana Lyrics
Mpigieni Bwana vigelegele, enyi wacha Mungu,
Kusifu kwawapasa *2 (wenye) wenye moyo mnyofu
- Enyi watumishi wa Bwana lisifuni,
lisifuni jina la Bwana
- Jina la Bwana litukuzwe,
Sasa na hata milele
- Toka mawio ya jua na hata machweo yake
Jina la Bwana lisifiwe
- Bwana ametukuka juu ya mataifa yote
Utukufu wake wazipita mbingu
- Nani ni sawa na Bwana,
Mungu wetu aketiye juu?
- Humwinua fukara kutoka mavumbini
Na kumkweza maskini kutoka unyonge