Mpokee Mtumishi Wako
| Mpokee Mtumishi Wako | |
|---|---|
| Performed by | St. Joseph Migori |
| Album | Nitachezacheza |
| Category | Kwaresma na Toba (Lent & Repentance) |
| Composer | Alfred Ossonga |
| Views | 26,930 |
Mpokee Mtumishi Wako Lyrics
- { Ee Mungu Baba Mwenyezi tuko hapa mbele zako,
Tunakulilia Baba utusikilize } *2Ipokee roho ya mwanao, mpokee mtumishi wako
Mpokee anakuja kwako, mpokee mtumishi wako,
Enyi malaika wa mbinguni, mchukue mpeleke kwa Baba,
Mchukue mpeleke kwa baba - Usiyakumbuke Baba makosa aliyotenda,
Umsamehe makosa ya ujana wake - Fariji roho za wote wanaohuzunika,
Uwape matumaini uwape tulizo - Ee Bwana ungehesabu, makosa ya wanadamu,
Ni nani angesimama mbele yako wewe - Ee Mungu mwenye rehema kumbuka rehema zako
Maana zimekuwapo tokea zamani