Mpokee Mtumishi Wako Lyrics

MPOKEE MTUMISHI WAKO

@ Alfred Ossonga

 1. { Ee Mungu Baba Mwenyezi tuko hapa mbele zako,
  Tunakulilia Baba utusikilize } *2

  Ipokee roho ya mwanao, mpokee mtumishi wako
  Mpokee anakuja kwako, mpokee mtumishi wako,
  Enyi malaika wa mbinguni, mchukue mpeleke kwa Baba,
  Mchukue mpeleke kwa baba

 2. Usiyakumbuke Baba makosa aliyotenda,
  Umsamehe makosa ya ujana wake
 3. Fariji roho za wote wanaohuzunika,
  Uwape matumaini uwape tulizo
 4. Ee Bwana ungehesabu, makosa ya wanadamu,
  Ni nani angesimama mbele yako wewe
 5. Ee Mungu mwenye rehema kumbuka rehema zako
  Maana zimekuwapo tokea zamani
Mpokee Mtumishi Wako
COMPOSERAlfred Ossonga
CHOIRSt. Joseph Migori
ALBUMNitachezacheza
CATEGORYKwaresma na Toba (Lent & Repentance)
 • Comments