Mshike Mshike
Mshike Mshike | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Mshike Mshike (Vol 5) |
Category | Tafakari |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 13,975 |
Mshike Mshike Lyrics
{ Hebu wanadamu na tufikirie sasa ni wapi tutakwenda,
Vita vimezidi amani hakuna shetani ametia nanga } *2
Mshike mshike kila kona watu wakimbilia usalama
Lo! Lo! hili jambo limekuwa kawaida
Ona wazee na watoto wateseka
Mshike mshike, mshike mshike
mshikeshike huu utaisha lini?
(Tumuombe Mungu), atikise huu mshikemshike- Ulimwengu wote umekuwa na visa vya ajabu,
Pande moja vita pande nyingine mambo ya ajabu
Tujisitiri wapi, kila pande machungu,
Tunakuomba ee Mwenyezi utupe usalama Baba - Watu nao wamekuwa wakali kuliko wanyama
Tunaishi kama hakuna kizazi kingine tena
Vita vya kila siku, uhasama wa mali,
Kizazi chetu kimekuwa dhiki tena ukiwa sana - Ulimwengu nao umekuwa jeneza la vijana,
Kuvaa vibaya madawa makali wanatumia
Eti wao wajanja, waenda na wakati
Hawajui maisha yana mwisho silaha yao pombe - Hebu fikiria unayefanya mambo haya yote,
Ujue ya kuwa kila lenye mwanzo linao mwisho,
Acha ya kidunia, faida ya ukiwa
Mtegemee Mungu unayo nafasi hii kabla hujafa