Mshipi
Mshipi | |
---|---|
Performed by | Kwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha |
Album | MSHIPI (VOL. 22) |
Category | Zaburi |
Composer | E. F. Jissu |
Views | 29,815 |
Mshipi Lyrics
Ni nani aliye Mungu, Mungu ila Bwana
Ni nani aliye mwamba, mwamba ila Mungu
{Ni Mungu ndiye anifungaye mshipi wa nguvu aha!
Ni Mungu ndiye kimbilio la unyonge wangu aha!
Naye anaifanya kamilifu njia yangu } *2- Ni yeye Bwana aliye nguvu zangu nampenda sana
Ni yeye Jabali langu na boma langu na Mwokozi wangu
Mungu wangu mwamba wangu ninayemkimbilia
Ngao yangu na pembe ya wokovu wangu
na ngome yangu - Katika shida zangu nilimwita Bwana ee Bwana
Na kumlalamikia Mungu ee Mungu
Akaisikia sauti yangu hekaluni mwake
Kilio changu kikaingia masikioni mwake - Bwana alinitendea sawasawa na haki yangu
Akanilipa sawasawa na haki yangu - Nitamwita Bwana astahiliye kusifiwa
Hivyo nitaokoka na adui zangu