Mshukuruni Mwokozi
   
    
     
         
          
            Mshukuruni Mwokozi Lyrics
 
             
            
- Mshukuruni Mwokozi enyi mataifa
 Pigeni vigelegele pigeni makofi
 Tangazeni rehema zake leo asubuhi
 Semeni ya kuwa Bwana ni mwenye adili
- Njooni tumwimbie Bwana, mwamba wa wokovu wetu
 Mikononi mwake zimo bonde za dunia
 Bahari ni yake ndiye aliyeiumba
 Na mikono yake alituumba sisi
- Bwana ametamalaki mataifa watasema
 Ameketi juu ya makerubi mbinguni
 Yeye Bwana katika Sayuni ni mkuu
 Katukuka juu ya mataifa yote
- Mshangilieni Bwana mwimbieni na zaburi
 Vinanda na baragumu vyote mpigieni
 Mshukuruni Bwana kwa kuwa ni mwema
 Kwa kuwa fadhili zake ni za milele