Msifuni Mungu Wenu

Msifuni Mungu Wenu
Performed bySt. Cecilia Mirerani
AlbumBaragumu la Maria
CategoryZaburi
ComposerG. C. Mkude
Views6,513

Msifuni Mungu Wenu Lyrics

  1. Msifuni Mungu wenu enyi viumbe vyake
    Pazeni sauti zenu, mmwimbie kwa furaha
    {Leteni ngoma (leteni), leteni kinanda leteni na zeze
    Pia na midomo ifunguke vinywa vyenu vifunuke
    Tumsifu (tumsifu) tumsifu, tumsifu Bwana
    Tumsifu Mungu wetu aliyetuumba}

  2. Kusanyeni viumbe vyote viumbe vyote vya duniani
    Vimuimbie kwa shangwe, virukeruke mbele za Bwana
  3. Tumieni ulimi wenu kwa kuvipiga vigelegele
    Mmwimbie kwa shangwe mrukeruke mbele za Bwana
  4. Kila kiumbe duniani na kifungue kinywa chake
    Kishangilie kwa nguvu na kimuimbie kwa furaha