Msifuni Mungu Wenu Lyrics

MSIFUNI MUNGU WENU

@ G. C. Mkude

Msifuni Mungu wenu enyi viumbe vyake
Pazeni sauti zenu, mmwimbie kwa furaha
{Leteni ngoma (leteni), leteni kinanda leteni na zeze
Pia na midomo ifunguke vinywa vyenu vifunuke
Tumsifu (tumsifu) tumsifu, tumsifu Bwana
Tumsifu Mungu wetu aliyetuumba}

  1. Kusanyeni viumbe vyote viumbe vyote vya duniani
    Vimuimbie kwa shangwe, virukeruke mbele za Bwana
  2. Tumieni ulimi wenu kwa kuvipiga vigelegele
    Mmwimbie kwa shangwe mrukeruke mbele za Bwana
  3. Kila kiumbe duniani na kifungue kinywa chake
    Kishangilie kwa nguvu na kimuimbie kwa furaha
Msifuni Mungu Wenu
COMPOSERG. C. Mkude
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMBaragumu la Maria
CATEGORYZaburi
  • Comments