Mtunze Ndoa
Mtunze Ndoa Lyrics
Mungu amewaunganisha
{ Mtunze ndoa hii yenu (kwa mapendo)
Mtunze ndoa hii yenu, mwanga wenu upendano } *2
- Mbele ya kanisa lake Mungu - mmeunganishwa ninyi
Pendo na amani ziwe kwenu - ndoa itakate hima
- Mume umpende mke wako - iwe fumbo lako tuzo
Mke umtunze mume wako - mbinguni katunukiwa.
- Vita na ugomvi vijitenge - omba radhi ukosapo
Choyo na anasa visiwepo - mwanga wenu upendano
- Nyumba ya amani lengo lenu - Kristu tegemeo lenu
Ndoa ni patano takatifu - timilifu kwake Mungu
- Mungu awajaze neema zake -m`barikiwe na watoto
Msiwapoteze wana wenu - wote mali yake Mungu