Mungu au Shetani

Mungu au Shetani
Performed bySt. Paul Students' Choir (University of Nairobi)
AlbumHabari Tuliyoleta (Vol 6)
CategoryTafakari
ComposerJ. C. Shomaly
Views9,510

Mungu au Shetani Lyrics

  1. Ndugu yangu sikia nasema kwa makini,
    Habari hii kuu ya ufalme wa Mungu
    Inasikika sana, sasa imeenea,
    Lakini sio wengi, wanaoiamini

    Waimbaji tumeshaimba nyimbo nyingi
    Makasisi wamehubiri pande nyingi
    { Twasema uokoke, nawe wasema kesho
    Inapofika kesho, wasema kesho kutwa
    Siku nazo zapita, miaka inapita
    Uchague mwenyewe, Mungu au shetani } *2

  2. Ukizipata shida, walaumulaumu,
    Ndugu na majirani, wadhani umelogwa
    Unaanza ugomvi, wachukia wengine,
    Hata bila sababu wawaita wachawi
  3. Waomba mara moja, ukikosa majibu,
    Kesho inapofika waenda kwa mganga
    Ngoja nikueleze, Mungu hana haraka,
    Jifunze vumilia majibu utapata
  4. Jifikirie ndugu, usingoje ya kesho,
    Muda ni wako sasa, amua ukubali
    Mengi tumeyasema, ilobaki ni kwako,
    Uchague mwenyewe, Mungu au shetani