Mungu Kaniita

Mungu Kaniita
Performed byKwaya Kuu ya St. Cecilia Arusha
AlbumMSHIPI (VOL. 22)
CategoryTafakari
ComposerF. Mtegeta
Views8,081

Mungu Kaniita Lyrics

  1. Tazama Mungu kaniita kati yao wanyonge
    nimtumikie yeye
    Tazama amenichagua kati ya viumbe
    nimuimbie yeye
    {Nitashangilia, sitaona haya,
    nitaruka kama ndama a haa
    Nami nitayatangaza bila woga
    matendo yake kwa mataifa } *2

  2. Mungu amenichagua, mimi amenichagua
    Tena akanitakasa na kunibariki, nimuimbie
  3. Furaha yangu kubwa, hii ni kuimba Nimwimbie
    Mungu wangu nyakati hizi za ujana ujana wangu
  4. Tujalie ujasiri, uvumilivu, wa kutangaza
    Neno lako Mungu kwao mataifa, wakufuate.
  5. Natarajia ushindi, siku ya mwisho, Nishangilie
    Na nifurahiye utukufu wako, milele yote