Mungu Wangu Nitakutukuza
Mungu Wangu Nitakutukuza | |
---|---|
Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) |
Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) |
Category | Zaburi |
Composer | J. C. Shomaly |
Views | 3,800 |
Mungu Wangu Nitakutukuza Lyrics
Mungu wangu nitakutukuza maana umeniinua,
Umesikia maombi yangu, sala zangu umenijibu
Na sasa ninafurahia, kwa jinsi ulivyonipenda,
Naimba ninachezacheza, ili kukushukuru wewe
Watu wote imbeni kwa furaha, pia na shangwe,
Pigeni vigelegele vya shangwe, pia makofi
{ Leteni kinanda (leteni leteni kinanda)
Leteni na zeze (leteni zeze)
Tumwimbie Bwana Mungu wetu yeye atupenda } *2- Mungu ninakushukuru kwa kuniumba mimi,
Umenipa na akili, Bwana ninashukuru - Ametupa na uhai pumzi yenye kutosha
Watu wote simameni, imbeni kwa furaha - Mungu nitakushukuru ningali bado hai
Na mwisho nifike kwako, nifurahi milele