Mvivu Wewe
   
    
     
         
          
            Mvivu Wewe Lyrics
 
             
            
- Mvivu wewe mvivu * 3 mvivu wewe
 Hebu watazame wadudu hawa
 Hebu watazame sisimizi wewe
 Wana adili ya kazi pasipo kusimamiwa
 (Tazama wanavyojituma (jituma) hawalazimishwi
 Tena hawana kiongozi (yeyote) wa kuwapangia)*2
 {Ewe mvivu utalala we! we! hatarini
 Utaondoka lini katika usingizi wako? }*2
- Kwa wenzako kunapokucha, wewe nd'o unalala
 Wenzako wanapoamka, wewe wajigeuza
 Wenzako wakipanga majukumu, wewe waota ndoto
 Wenzako wanapotoka kazini, wewe watupa shuka
- Wenzako wanafanya kazi, tena kwa kujituma
 Wenzako wanafanya kazi, tena kwa moyo mmoja
 Daima wewe wajivuta, tena wingi wa maneno
 Hata nazo salamu haziishi, tena sababu mia mia.
- Hebu jitazame sasa, umbeya wakutawala,
 Tena ukijichunguza, na wizi wakuandama
 Wenzako wakifanikiwa, waanza kazi kuwaomba,
 Na maisha ya jirani, wewe wayafuatilia
- Jiulize utabarikiwa, lini ewe mvivu,
 Jiulize utaamka, lini ewe mvivu,
 Ukishiba leo huwazi, ya kesho utakula nini
 Hakuna lolote ufanyalo bila ya kusimamiwa.