Mvivu Wewe Lyrics

MVIVU WEWE

@ E. A. Minja

Mvivu wewe mvivu * 3 mvivu wewe
Hebu watazame wadudu hawa
Hebu watazame sisimizi wewe
Wana adili ya kazi pasipo kusimamiwa
(Tazama wanavyojituma (jituma) hawalazimishwi
Tena hawana kiongozi (yeyote) wa kuwapangia)*2
{Ewe mvivu utalala we! we! hatarini
Utaondoka lini katika usingizi wako? }*2

 1. Kwa wenzako kunapokucha, wewe nd'o unalala
  Wenzako wanapoamka, wewe wajigeuza
  Wenzako wakipanga majukumu, wewe waota ndoto
  Wenzako wanapotoka kazini, wewe watupa shuka
 2. Wenzako wanafanya kazi, tena kwa kujituma
  Wenzako wanafanya kazi, tena kwa moyo mmoja
  Daima wewe wajivuta, tena wingi wa maneno
  Hata nazo salamu haziishi, tena sababu mia mia.
 3. Hebu jitazame sasa, umbeya wakutawala,
  Tena ukijichunguza, na wizi wakuandama
  Wenzako wakifanikiwa, waanza kazi kuwaomba,
  Na maisha ya jirani, wewe wayafuatilia
 4. Jiulize utabarikiwa, lini ewe mvivu,
  Jiulize utaamka, lini ewe mvivu,
  Ukishiba leo huwazi, ya kesho utakula nini
  Hakuna lolote ufanyalo bila ya kusimamiwa.
Mvivu Wewe
COMPOSERE. A. Minja
CHOIRSt. Cecilia Mirerani
ALBUMMchanganyo
CATEGORYTafakari
 • Comments