Mwalimu Tazama

Mwalimu Tazama
Performed by-
CategoryMafundisho ya Yesu
ComposerJ. C. Shomaly
Views3,077

Mwalimu Tazama Lyrics

  1. Mwalimu, tazama,
    huyu amepatikana ana dhambi
    anapaswa kupigwa mawe
    Kama sheria ilivyoandikwa
    na yapaswa yeye kufa mawe

    [b] Bwana Yesu akasema
    |s| Ni nani yeye asiye na dhambi ampige jiwe *2
    Ni nani yeye nasema ni nanii*2

    |a| Ni nani yeye asiye na dhambi ampige jiwe *2
    Hakuna nasema, hakuna nasema *2

    |t| Ni nani yeye asiye na dhambi ampige jiwe *4

    |b| Ni nani yeye asiye na dhambi ampige jiwe
    Ni nani yeye ni nani ni nani, ni nani ni nani
    Ni nani, ni nani ni nani, ni nani ni nani*2

    Wa -ka -shi -kwa -na -bu -twa -a!
    Wakayatupa mawe chini na kwa aibu wakaenda zao

  2. Walitazama tazama, hakukuwa naye mtu
    Aliyekuwa tayari aweze kurusha jiwe
    Yesu naye akasema, kamwambia mama yule
    Inuka uende zako, usitende dhambi tena
  3. Somo hili lafundisha na sisi tusiwe mbele
    Kuwahukumu wenzetu, kujiona sisi wema
    Tujinyenyekeze chini, tusijinyanyue juu
    Yeye Mungu mwenye haki atatusamehe dhambi