Mwili wa Bwana Yesu
   
    
     
         
          
            Mwili wa Bwana Yesu Lyrics
 
             
            
- Mwili wa Bwana Yesu, chakula cha mbingu
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
 
 Hima uwe nasi ee Bwana Yesu
 Ukatushibishe chakula bora
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
- Yesu alituambia, Yeye ni chakula
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
 
 Anilaye mimi na kunywa damu
 Anao uzima wa siku zote
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
- Yesu alituambia, kuwa tumpokee
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
 
 Sote twaamini, ni mwili wake
 Pia twaamini ni damu yake
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
- Hii ndiyo karamu, aliyotuachia
 Ni chakula cha roho, chenye uzima
 
 Ee Bwana Mwokozi tunakuomba
 Kwa chakula hiki tuimarike
 Ni chakula cha roho, chenye uzima