Mwimbieni Bwana
Mwimbieni Bwana Lyrics
Mwimbieni Bwana, mataifa ya dunia
Mwimbieni Bwana litukuzeni jina lake
- Tangazeni wokovu wake siku kwa siku
Yaelezeni mataifa utukufu wake
- Utukufu na uzuri unamtangulia, Enzi na
wangavu zimo katika kikao chake kitakatifu
- Mpeni Bwana enyi jamii za mataifa
Mpeni Bwana sifa na enzi
- Mpeni Bwana utukufu wa jina lake
Toeni sadaka ingieni katika sebule zake
- Semeni kati ya mataifa, Bwana ni mfalme
- Atatawala ulimwengu kwa haki
Na mataifa kwa uaminifu wake
- Atukuzwe Baba na mwana, na Roho Mtakatifu
kama mwanzo na sasa, na siku zote milele.
Amina.