Mwimbieni Mwimbieni Bwana
| Mwimbieni Mwimbieni Bwana | |
|---|---|
| Performed by | St. Paul Students' Choir (University of Nairobi) | 
| Album | Tazameni Miujiza (Vol 2) | 
| Category | Entrance / Mwanzo | 
| Composer | J. C. Shomaly | 
| Views | 6,814 | 
Mwimbieni Mwimbieni Bwana Lyrics
- Mwimbieni,
 Mwimbieni Bwana, mwimbieni Bwana,
 Mwimbieni, mwimbieni Bwana wimbo mpya,
 Kwa maana,
 Ametenda Bwana, mambo ya ajabu,
 Kwa maana Bwana ametenda maajabu,
 { Inueni sauti zenu, imbeni kwa furaha
 Imbeni na zaburi mshangilieni Mwokozi } *2
- Mkono wa kuume, mkono wake mwenyewe
 Mkono wake wa kuume umetenda wokovu
- Ameufunua, Bwana amefunua
 Wokovu wake machoni kwa mataifa yote
- Miisho yote, miisho ya dunia
 Imeuona wokovu, wokovu wake Bwana
 
  
         
                            